Jinsi ya kujitambulisha kwa Kiswahili(how to introduce yourself in Swahili)
Karibu kwenye makala yetu mpya! Leo, tutajifunza jinsi ya kujitambulisha kwa lugha ya Kiswaili. Iwe unasafiri kwenda Afrika Mashariki, unafanya biashara na wazungumzaji wa lugha ya kiswahili, au una nia tu ya kujifunza lugha hii nzuri, kujua jinsi ya kujitambulisha kwa usahihi ni hatua muhimu ya kwanza. Katika makala hihi tutakuongoja hatua kwa hatua kupitia misemo muhimu na mazungunzo rahisi ili uweze kujiamini unapokutana na watu wapya wanaozungumza lugha ya Kiswahili.
Welcome to our new article! Today we will look at how to introduce yourself in the Swahili language. Whether you are traveling to East Africa, doing business with Swahili speakers, or are simply interested in learning this beautiful language, knowing how to introduce yourself correctly is an important step. In this article we will guide you step-by-step through important phrases and simple conversation so that you can feel confident when you meet new Swahili-speaking people. Keep reading to learn!
Dialogue
George anajitambulisha kwa Zakaria(George introduces himself to Zakaria)
George: Shikamoo mzee!
Zakaria: Marahaba, hujambo?
George: Sijambo, mimi ninaitwa George. Na wewe unaitwa nani?
Zakaria: Mimi ninaitwa Zakaria. Wewe ni raia wa nchi gani?
George: mimi ni mmarekani. Ninatoka marekani, jimbo la Michigani.
Zakaria: Karibu sana Tanzania.
George: Asante sana. Wewe ni mtanzania?
Zakaria: Ndiyo! Mimi ni mtanzania. Ninatoka Arusha.
George: Asante sana, nimefurahi kukutana na wewe!
Zakaria: Nimefurahi pia. Kwaheri na karibu tena.
MSAMIATI(VOCABULARY)
Kiswahili/Swahili English
Nomino Nouns
Arusha A city in the Northern Tanzania
jimbo(ma-) State(s)
Marekani America
Michigan A state in the United states of America.
Mmarekani(wa) American(s)
Mzee Elder/old person
nchi Country/nation
raia Citizen
Vitenzi Verbs
itwa be called
toka come from
Semi Expressions
Shikamoo(greeing) I give you respect
Marahaba(greeting) I accept your respect
Ndiyo positive response(yes)
hujambo?(greeting) How are you?
Sijambo(greeting) I am fine/well
Karibu sana You are very welcomed
Nimefurahi I am happy
kukutana to meet
Viulizi Interrogatives
Gani? which/what?
Nani? Who?
MAELEZO YA SARUFI (GRAMMAR NOTES)
(a) Viwakilishi nafsi.(personal pronouns prefixes)
Persons |
Example in word |
|
1st person (ni) |
ni-na-toka |
ninatoka |
2nd person (u) |
u-na-toka |
unatoka |
3rd person (a) |
a-na-toka |
ninatoka |
(b) Vivumishi vimilikishi(posessive adjectives)
Persons |
Pronoun |
Posessive adjectve |
example |
|
1st person |
mimi |
-angu |
Jina langu |
mine |
2nd person |
wewe |
-ako |
Jina lako |
yours |
3rd person |
yeye |
-ake |
Jina lake |
his/hers |
(c) Kitenzi kuwa katika njeo ya wakati uliopo. (the verb to be (is/am/are) in the present tense.
ni(positive) si(negative)
mimi ni mtanzania mimi si mtanzania
wewe ni mtanzania wewe si mtanzania
yeye ni mtanzania yeye si mtanziania.
(d) Utaifa (Nationality)
The prefix M-is attached to the name of the country to form nationality
Examples
Country Nationality
Tanzania Mtanzania
Ujerumani Mjerumani
marekani Mmarekani
Hivi ndivyo unavyoweza kujitambulisha kwa Kiswahili! Tunatumai umefurahia kujifunza misingi hii muhimu ya mawasiliano kwa kiswahili. Endelea kufanya mazoezi, na hivi karibuni utakuwa unazungumza kwa ujasiri zaidi. Asante kwa kusoma.
So, that is how you can introuce yourself in Swahili! We hope you enjoyed learning these basics of communication in Swahili. Keep practicing and soon you will be speaking with more confidence. Thank you for reading.
Comments